Katika bonde la kijani lililojaa mandhari ya kuvutia kusini mwa Tanzania, wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma sasa inang’aa kama nyota mpya ya utalii.
Kupitia uwekezaji wa
Shilingi bilioni 2.1 kutoka Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia
Suluhu Hassan, fedha hizo zimetumika kujengamiundombinu ya Hifadhi ya Taifa ya
Nyerere ikiwemo lango la kisasa kuingia Hifadhi ya Taifa ya Nyerereambalo
limejengwa eneo la Likuyuseka Maganga na sasa, ndio mlango rasmi wa watalii
kuingia hifadhi hiyo kupitia Nyanda za Juu Kusini.
Akizungumza kwa
furaha hivi karibuni, Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo, Mhe. Ngollo Malenya, anasema
ujenzi wa lango hilo umekamilika na sasa wilaya yake ipo tayari kuwakaribisha
wageni kutoka kila pembe ya ukanda wa kusini,ikiwemo mikoa ya Lindi, Mtwara,
Njombe, Iringa, Mbeya hadi Ruvuma, na hata nchi jirani kama Msumbiji na Malawi.
“Lango hili ni fursa
ya kipekee kwa Namtumbo na Mkoa wa Ruvuma. Linakuza uchumi wetu kwa haraka na
linafungua njia ya uwekezaji mkubwa kwenye sekta ya utalii,” anasisitiza
Malenya huku akitoa rai kwa wawekezaji wa ndani na nje kuwekeza kwenye ujenzi
wa hoteli, huduma za utalii na miundombinu mingine muhimu.
0 Maoni