Wakala wa Usajili wa
Biashara na Leseni (BRELA) imetoa gawio la Shilingi Bilioni 20.4 kwa Serikali
kwa mwaka 2025, likiwa ni ongezeko kutoka Shilingi Bilioni 18.9 zilizotolewa
mwaka 2024.
Gawio hilo limetolewa
leo Ikulu jijini Dar es Salaam na kupokelewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika hafla ya kupokea gawio na
michango kutoka kwa taasisi na mashirika ya umma.
Vilevile, BRELA
imepokea tuzo kama Taasisi iliyofanya vizuri katika kuchangia gawio kila mwaka,
kwa wastani wa Shilingi Bilioni 16.8 kwa kipindi cha miaka mitano mfululizo.
Hafla hiyo
imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali na taasisi husika, wakiwemo
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya BRELA, Prof. Neema Mori, pamoja na Afisa
Mtendaji Mkuu wa BRELA, Bw. Godfrey Nyaisa.
0 Maoni