Kampuni ya Twiga Minerals Corporation imekuwa kinara katika kuchangia gawio kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali kwa kampuni za biashara ambapo imetoa gawio la shilingi bilioni 93.6.
Kampuni ya Airtel
Tanzania imekuwa mchangiaji wa pili kwa kuchangia fedha kwenye Mfuko Mkuu wa
Serikali ambapo imetoa gawio la shilingi bilioni 73.9
Nafasi ya tatu
imechukuliwa na Benki ya NMB kwa kutoa gawio la shilingi bilioni 68.1
Kampuni zingine
zilizotoa gawio kubwa mwaka huu chini ya taasisi zilizotajwa hapo juu ni pamoja
na Kampuni ya Puma Energy iliyotoa gawio la shilingi bilioni 13.5.
Nyingine ni Shirika
la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) iliyotoa gawio la shilingi bilioni 11
pamoja Benki ya Kitaifa ya Biashara NBC iliyotoa gawio la shilingi bilioni
10.5.
Hayo yamebainika leo
Juni 10, 2025, Ikulu, Dar es Salaam, wakati wa hafla ya kupokea gawio na
michango kutoka kwa mashirika na taasisi za umma ambapo mgeni rasmi alikuwa
Rais Samia Suluhu Hassan.
0 Maoni