Katika kuelekea
kuanza kwa msimu mpya wa utalii (high season) Juni, 2025, Hifadhi ya Taifa
Ruaha imeendesha kikao maalumu kilichowakutanisha wadau wa utalii ili
kujadili Masuala mbalimbali kuhusu
shughuli za Utalii,changamoto na mikakati ili kukuza utalii ndani na nje ya
Hifadhi ya Taifa Ruaha.
Kikao hicho cha siku
moja kilichofanyika jana Mei 30, 2025 katika Ukumbi wa Sunset Hotel mjini
Iringa kimewajumuisha TANAPA, Mawakala wa Utalii, waongoza watalii (Guides),
Mawakala wa Usafirishaji, wamiliki wa hoteli, wawakilishi kutoka Bodi ya Utalii
Tanzania (TTB), Wizara ya Maliasili na Utalii-Kusini, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa,
Uhamiaji na Polisi.
Akielezea umuhimu wa
kikao hicho Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi na Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Ruaha
Abel Mtui alisema, “Wadau wote
waliojumuika katika kikao hicho ni muhimu katika mnyororo mzima wa utalii ili
kufikia maazimio ya pamoja katika kukuza sekta ya utalii Nyanda za juu Kusini
na Tanzania kwa ujumla.
Aidha, Kamishna Mtui
aliwaeleza washiriki wa kikao hicho mipango na mikakati mbalimbali ambayo
hifadhi imejiandaa kuitekeleza kuhakikisha watalii wanapata huduma bora
kulingana na thamani ya fedha zao, na alisisitizi kufanyia kazi maoni na
ushauri uliotolewa na wadau hao.
Hifadhi ya Taifa
Ruaha ni miongoni mwa Hifadhi za Taifa 21 zinazosimamiwa na Shirika la Hifadhi
za Taifa Tanzania (TANAPA) ambayo inapatikana katika mikoa ya Iringa, Dodoma na
Mbeya ikiwa na ukubwa wa kilometa za mraba 19,822 ikisifika kwa kuwa na idadi
kubwa ya Simba barani Afrika.
Na. Jacob Kasiri -
Iringa
0 Maoni