Shirika la Hifadhi za
Taifa (TANAPA) limetunukiwa tuzo ya hadhi ya juu kwa mara ya sita mfululizo
iitwayo European Quality Choice Diamond ya mwaka 2025 katika hafla iliyofanyika
usiku wa tarehe 29 Mei, 2025, jijini Stockholm, nchini Uswidi, kwa kutambua utendaji
wake mahiri katika utalii na uhifadhi.
Tuzo hiyo
ilikabidhiwa na Mshauri Mtendaji Mkuu wa taasisi ya European Society for
Quality Research (ESQR), Bw. Michael Harris,
kwa Balozi wa Tanzania nchini Uswidi, Mhe. Mobhare Matinyi, ambaye
aliambatana na Kamishna wa Uhifadhi wa TANAPA, Bw. Mussa Nassoro Kuji; Kamishna
Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi, Rodwell Ole Meing'ataki; Afisa Mkuu wa
Uhifadhi, Eunice Msangi; Afisa Uhifadhi Andrew Mbai; na Afisa Mwandamizi wa
Ubalozi wa Tanzania, Malik Hassan.
TANAPA ilikuwa
kampuni pekee ya utalii na uhifadhi kati ya 49 kutoka nchi 42 duniani zikiwemo
zingine sita za Afrika iliyotunukiwa tuzo hiyo. TANAPA ni moja ya taasisi
kadhaa nchini zenye usajili wa ISO 9001:2015 ambacho ndicho kigezo cha kupimwa
utendaji na ESQR kila mwaka.
0 Maoni