Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary S. Senyamule Mei14, 2025
amekabidhiwa tuzo ya Mwanamke kinara Kanda ya Kati kutoka ‘Central Women
Connect, Mwanamke Kinara Awards’ ambao ni waandaaji wa tuzo hizo,ambapo
makabidhiano yamefanyika nje ya ofisi yake (Jengo la Mkapa).
Tuzo hizo za Dr. Samia Mwanamke Kinara, ni tuzo
zilizoandaliwa kwa ajili ya kutambua nguvu ya mwanamke kwenye jamii ambapo
Zilitolewa tarehe 10/5/2025 katika ukumbi wa Lavenda Hotel Jijini Dodoma.
“…Hii tuzo ni ya wanawake wote wa Mkoa wa Dodoma ,twendeni tukaonyeshe kuwa Wanawake tunaweza, na kuwa mstari wa mbele kwa kuboresha taarifa kwenye Daftari la kudumu la mpiga kura ili tupate nafasi ya kupiga kura,” amesema Mhe. Senyamule.
Akizungumza kabla ya kukabidhi tuzo hiyo kwa Mkuu wa
Mkoa,Mratibu wa ‘Central Women Connect Mwanamke Kinara Awards’ Bi. Rashida
Mfaume amesema sababu za kumtunuku tuzo hiyo ya viwango vya juu na ambayo
haishindaniwi, ni kutokana na heshima aliyonayo kama Mwanamke Kiongozi kwa
kusimamia vyema miradi ya kimkakati.
“Kazi umeiendeleza katika sekta mbalimbali za maendeleo ndani ya Mkoa huu, zikiwepo usimamizi wa miradi, kuna ambayo imeshakamilika na mingine bado inaendelea, hivyo tunajivunia wewe, na unastahili kuwa mshindi wa tuzo hii,” Bi. Mfaume.



0 Maoni