Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Profesa Mohamed Yakub Janabi ameshinda nafasi ya Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) kanda ya Afrika.
Prof. Janabi ambaye pia ni Mshauri wa Rais wa Tanzania
Masuala ya Afya na Tiba ametangazwa rasmi kushinda kwa kishindo nafasi hiyo kwenye
uchaguzi uliofanyika leo Mei 18, 2025 jijini Geneva nchini Uswisi.
Uchaguzi huo umefanyika kuziba nafasi ambayo iliachwa wazi na aliyekuwa Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO) kanda ya Afrika, Dkt. Faustine Ndugulile baada ya kufariki dunia Novemba 27, 2024.
Prof. Janabi alikuwa ni Mgombea pekee kutoka nchi za kusini mwa jangwa la Sahara, huku wenzake wanne wakitokea nchi za Afrika Magharibi akiwemo Dkt. N’da Konan Michel Yao (Ivory Coast), Dkt. Dramé Mohammed Lamine (Guinea), Dkt. Boureima Hama Sambo (Niger) na Prof. Mijiyawa Moustafa wa Togo.
0 Maoni