Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais- TAMISEMI, Mhe. Mohamed
Mchengerwa ameshiriki
kwenye zoezi la kuboresha taarifa
zake kwenye Daftari la Kudumu la Mpiga Kura Ikwiriri - Rufiji.
Mara baada ya kuboresha taarifa zake jana Mei 20, 2025, Mhe. Mchengerwa
amewataka wananchi kote nchini kutumia muda wa siku mbili zilizobaki kuboresha taarifa zao.
"Naomba kutoa wito kwa wananchi kwenda kuboresha
taarifa zao katika kipindi hiki kifupi cha siku mbili ili waweze kupata haki
yao ya msingi ya kupiga kura kwa maendeleo ya taifa letu," amesisitiza Mhe Waziri Mchengerwa.
Aidha, amefafanua kuwa zoezi la kuboresha taarifa ni la
muhimu kwa kuwa taarifa hizo zinaweza pia kutumika na Serikali ili kuleta
maendeleo.
Pia Waziri Mchengerwa ametoa wito kwa watanzania kutumia vizuri hali yao ya kupiga kura wakati utakapofika.




0 Maoni