Rais wa Jamhuri ya Finland Mhe. Alexander Stubb afurahishwa
na uhifadhi wa historia uliohifadhiwa katika kituo cha Makumbusho na Nyumba ya
Utamaduni.
Akiongea katika ziara maalum aliyoifanya kituoni hapo, Mhe.
Rais Stubb amesema “kwa sasa natambua chimbuko langu (Now, I know where I came
from)”, kauli ambayo imetokana na kujionea historia adhimu ya chimbuko la
mwanadamu.
Naye mwenyeji wake Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb), Waziri
wa Maliasili na Utalii amekumbushia ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania
na Finland ni wa kihistoria kwa kutaja ushahidi wa marais waliopita kutoka
Tanzania kutembelea Finland kuanzia Rais wa kwanza Mwl. JK Nyerere, Rais Benjamin
Mkapa, Rais Jakaya Kikwete na hatimaye Rais Samia Suluhu Hassan.
Aidha, Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa la Tanzania Dkt. Noel Lwoga amewahimiza watanzania na wadau mbalimbali kutembelea maeneo ya Makumbusho na Malikale ili kufahamu historia na asili yao.

0 Maoni