Naibu Waziri Mkuu na
Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amekutana na kufanya mazungumzo na
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Nishati ya PUMA Energies, Duniani Bw. Mark Russell.
Katika mazungumzo
hayo yaliyofanyika Mei 27, 2025 jijini Dodoma, Dkt. Biteko ameipongeza Kampuni
ya PUMA Energies kwa kuwekeza nchini na kutoa huduma ya viwango vya juu katika
bidhaa zake pamoja na kuzingatia wazawa katika nafasi za juu za utendaji za
Kampuni hiyo nchini.
Vilevile, ametoa rai
kwa PUMA Energies kuendelea kuwekeza zaidi nchini na kusema kuwa Kampuni hiyo
inaweza kujenga vituo zaidi vya kuweka gesi kwenye magari ili kusaidia
upatikanaji wa huduma kwa wananchi.
Kuhusu nishati safi
ya kupikia, Dkt. Biteko ametoa wito kwa Kampuni ya PUMA kuwekeza katika eneo
hilo na kusema kuwa Serikali itaendelea kuimarisha ushirikiano wake kwa Kampuni
hiyo.
Naye, Mtendaji Mkuu
wa Kampuni ya Nishati ya PUMA Energies, Bw. Mark Russell amesema kuwa Kampuni
yake imewekeza zaidi ya dola za kimarekani milioni 24 kwa ajili ya ujenzi wa
vituo vitatu vya kujaza gesi kwenye magari katika mikoa ya Dar es salaam na
kimoja Dodoma.
Na. Ofisi ya Naibu
Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati





0 Maoni