Jeshi la Polisi Mkoa wa
Mbeya kwa kushirikianana Askari wa Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori Tanzania (TAWA)
linamshikilia Riziki Charles Mapila (55) mkazi wa Lubele Wilaya ya Kyela akiwa na
nyara za Serikali vipande tisa vya meno ya tembo bila kibali.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa
Mbeya SACP Benjamin Kuzaga amesema mtuhumiwa alikamatwa Aprili 14, 2025 na
Askari waliokuwa doria katika Kitongoji cha Isaki, Kata ya Njisi, Tarafa ya
Unyakyusa, Wilaya ya Kyela akiwa na vipande hivyo 9 vya meno ya tembo vyenye uzito
wa kilogram 34.6 akiwa amehifadhi ndani ya mfuko wa sandarusi kisha kuficha porini.
Wakati huo huo, Jeshi la
Polisi Mkoa wa Mbeya kwa kushirikianana Askari wa TAWA Wilaya ya Mbarali linamshikilia
Kenedy Yawaga (37) Mkazi wa Itamba akiwa na nyara za Serikali vipande vitatu
vya meno ya tembo bila kibali.
Mtuhumiwa alikamatwa Aprili
03, 2025 katika Kijiji cha Mabadaga kilichopo Kata ya Mapogoro, Tarafa ya
Rujewa, Wilaya ya Mbarali, Mkoani Mbeya katika oparesheni maalum dhidi ya
wahujumu uchumi wa Taifa akiwa na nyara hizo zenye uzito wa kilogram 12 akiwa amefunga
kwenye mfuko wa sandarusi na kishakufukia ardhini kwenye shamba lake lililopo kwenye
mji wake.
Kamanda Kuzaga amesema
kwamba uchunguzi wa awali umebaini kuwa watuhumi wawali kuwa wanajihusisha na uwindajiharamu
katika Hifadhi za Taifa, taratibu za kuwafikisha Mahakamani zinaendelea.
0 Maoni