MWANASHERIA Mkuu wa Serikali
Hamza Johari amesema wanamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo
amekuwa akikilea Chama cha Mawakili wa Serikali nchini (PBA), na kukiwezesha
kuwa imara.
Mwanasheria Mkuu wa
Serikali, ametoa pongezi hizo, leo Aprili 14, 2025 wakati akifungua Mkutano
Mkuu wa mwaka wa PBA ambao ni wa tatu, uliofanyika katika ukumbi wa Jakaya
Kikwete Jijini Dodoma.
Alisema kuwa kaulimbiu ya
mwaka huu inasema, "Utawala wa Sheria katika utekelezaji wa majukumu ya
serikali ni nguzo muhimu katika kufikia Malengo ya Dira ya Taifa ya
Maendeleo 2050"
Mwanasheria Mkuu wa Serikali
Johari," Amesema, "Kaulimbiu hii inatukumbusha namna bora ya
ufanyajikazi kwa weledi na tayari imeshatengenezwa mpango mkakati ambao
utatekelezwa kwa moyo na hali ya juu na pia ni mpango unaoishi na kila baada ya
muda tutakuwa tunaitana kujitathmini tulipofikia."
Mwanasheria Mkuu wa
Serikali, Johari amewataka Mawakili wa Serikali kuhakikisha wanatumia ipasavyo
kliniki za ushauri wa Sheria kwa kutoa elimu ya sheria zilizopo katika ngazi za
mikoa na wilaya katika kutoa elimu ya masuala husika kwa jamii.
Pia ameiomba Serikali
kuendelea kuiongezea bajeti Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili iweze
kutekeleza majukumu yake kikamilifu.
Mwanasheria Mkuu huyo wa
Serikali amesema kumekuwa na changamoto ya ufinyu wa bajeti katika ofisi yake
pamoja na vitengo vyake hasa katika Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, jambo
ambalo limekuwa likiathiri kliniki za kisheria katika mikoa na wilaya.
0 Maoni