Rais wa Awamu ya Nne na
Mjumbe Maalum wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete
amewasilisha Ujumbe Maalum kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Congo (Congo
Brazzaville), Mhe. Collinet Makosso Anatole. Mhe. Anatole alipokea ujumbe huo wa maandishi kwa niaba ya Rais wa
Jamhuri ya Congo , Mhe. Denis Sassou Nguesso ambaye alikuwa kijijini kwao
kushiriki mazishi ya kaka yake.
Tukio hilo lilifanyika
jijini Brazzaville jana Aprili 14, 2025 na kushuhudiwa na baadhi ya maafisa
waandamizi wa nchi zote mbili.
Mhe. Kikwete aliwasilisha
pia salamu za Rais Samia ambazo zilielezea umuhimu wa nchi za Afrika kuimarisha
ushirikiano wa kiuchumi kama njia muhimu kwa bara hilo kujitegemea, hususan
katika kipindi hiki ambapo misaada kutoka nchi za magharibi imepungua
kwa kiasi kikubwa.
0 Maoni