Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania
Bara, Stephen Wasira, amekutana na kufanya mazungumzo na Askofu wa Kanisa la
Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Karagwe, Dk. Benson Bagonza,
wilayani Karagwe, mkoani Kagera.
Viongozi hao wawili walikutana jana, wakati wa ziara ya Wasira mkoani Kagera, ambako anakagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025, kusikiliza changamoto za wananchi na kuhutubia mikutano ya hadhara.
0 Maoni