Mamlaka ya
Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) imeandaa tuzo maalum kwa waandishi wa habari ambao
wameripoti taarifa na kuandaa makala mbalimbali kuhusu kazi na majukumu ya TMDA
katika kipindi cha kuanzia Julai, 2024 hadi Machi 2025.
Taarifa
iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa TMDA imesema lengo la tuzo hizo ni kutambua
mchango wa waandishi wa habari na kuleta hamasa katika kuelimisha jamii kuhusu
masuala ya udhibiti wa dawa, vifaa tiba, vitandanishi na bidhaa za tumbaku
kupitia vyombo vya habari ili kulinda afya ya jamii.
Kazi
zinazolengwa ni zile zilizoripotiwa kupitia Runinga (TV), Redio, Magazeti na Mitandao
ya Jamii kwa kipindi tajwa, ambapo baada ya kupokelewa zitashindanishwa na
hatimaye kuwapata washindi watakaopewa tuzo.
TMDA
inawaalika waandishi kuwasilisha kazi zao kabla ya kufika tarehe 18 Aprili,
2025 kupitia anuani ya barua pepe ya commpedtmda@gmail.com au kwa njia ya CD
katika ofizi za TMDA zilizopo Dodoma, Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Mtwara, Tabora
na Geita.

0 Maoni