Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia
Suluhu Hassan amesema Serikali inaendelea kubuni mbinu mbalimbali za
kukabiliana na wanyamapori wakali na waharibifu huku akiiielekeza Wizara ya
Maliasili na Utalii kuangalia namna ya kupitia upya kanuni za malipo ya kifuta
jasho/machozi.
Ameyasema hayo leo Februari 24, 2025 katika ziara alipokuwa
akizungumza na wananchi kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga .
"Tunaendelea kuongeza Askari Wanyamapori na kubuni
mbinu mbalimbali za kufukuza wanyama ikiwemo kutumia ndegenyuki (drones)"
Rais Samia amesisitiza.
Mkutano huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali wakiwemo Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb), Naibu Waziri, Mhe. Dunstan Kitandula (Mb), Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi pamoja na baadhi ya Watendaji kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii na Taasisi zake.




0 Maoni