Rais Samia afungua jengo nzuri la Halmashauri ya Bumbuli

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amefungua jengo jipya la kisasa la Halmashauri ya Bumbuli, katika siku yake ya pili ya ziara yake mkoani Tanga.

Akiongea leo Februari 24, 2025 Rais Dkt. Samia amenonekana kuvutiwa na jengo hilo na kusema kwamba ni jengo zuri linalofurahisha machoni lakini kubwa zaidi ni kuzogeza huduma kwa wananchi.

Dkt. Samia amewataka wananchi kulitunza jengo hilo kwa kuwa ni mali yao na kutoa wito kwa wafanyakazi Halmashauri watoe huduma nzuri kwa wananchi zinalingana na uzuri wa jengo hilo.

Pamoja na mambo mengine Rais Dkt. Samia amesema alimpiga kofi Mbunge wa Bumbuli, Mhe. January Makamba, na akamfichia chakula kama ulivyo uhusiano wa mama na mwana.

Akizungumza mbele ya wananchi wa Lushoto, Tanga, Rais Samia alimuita Makamba mbele ya hadhara na kumkumbatia, akieleza kwa mfano wa kifamilia jinsi alivyosimamia uhusiano wao.

Awali mbunge wa Bumbuli Mhe. January Makamba amemshukuru Rais Dkt. Samia kwa kumuamini na kumteua katika nafasi kadhaa wakati uliopita ikiwamo kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki na Waziri wa Nishati, akisema suala hilo limesalia kuwa historia isiyofutika katika maisha yake.




Chapisha Maoni

0 Maoni