Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein
Ali Mwinyi ameeleza kuridhishwa na
upatikanaji wa Bidhaa za Vyakula na kuwataka Wafanyabiashara Kutopandisha
Bei wakati Ramadhani itakapoanza.
Rais Dkt. Mwinyi amesema hayo alipotembelea Masoko ya Jumbi
, Mwanakwerekwe na Darajani kuangalia
Mwenendo wa Biashara na Upatikanaji wa
Bidhaa za Vyakula kuelekea Mwezi Wa
Ramadhani.
Aidha,Rais Dkt. Mwinyi
ameeleza kuwa Serikali inajipanga kwa ajili ya Ujenzi wa Masoko mengine
maeneo mbalimbali ili kila Mfanyabiashara afanye biashara kwenye mazingira rasmi .
Kuhusu Suala la Usafi
wa Masoko ameuagiza Uongozi wa Masoko hayo kutafuta njia Bora zaidi ya Uhifadhi
wa Bidhaa za Wafanyabiashara ili Masoko kuwa safi wakati wote.
Amezielekeza Taasisi zinazosimamia Masoko hayo kuhakikisha
Upatikanaji wa Huduma ya Maji na Vipooza hewa katika Masoko yote
pamoja na kuimarisha usafi.
Ziara hiyo ya Rais Dkt. Mwinyi ni ya kwanza tangu kufunguliwa kwa Masoko Mapya ya Jumbi , Mwanakwerekwe na Ukarabati Mkubwa wa Soko la Darajani.
0 Maoni