Upatikanaji wa nishati ya umeme kwa kutumia umemejua (solar energy) katika Kisiwa cha Rukuba kilichopo katika jimbo la Musoma Vijijini unatarajiwa kuwa mkombozi mkubwa maendeleo ya kisiwa hicho.
Katika kufanikisha jitihada hizo tayari Kituo cha Afya cha Kisiwa cha Rukuba kimefungiwa mfumo wa umemejua (solar energy) wenye thamani ya Tsh 345,600,000.
Taarifa iliyotolewa na mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Prof. Sospeter Muhongo imesema sehemu nyingine za kisiwa hicho zitafungiwa umemejua (solar energy).
Umeme huo utafungwa kupitia mradi mkubwa wa kufungia
umemejua kwenye visiwa vya nchi nzima vilivyoko Bahari ya Hindi na naziwa yetu
makuu, imeeleza taarifa hiyo.
“Kwa hiyo, Kisiwa cha Rukuba nacho kipo ndani ya mradi ambao
matayarisho yake yanakamilishwa, kwa mujibu wa taarifa kutoka REA kwenda kwa
Mbunge wa Jimbo.”
Baada ya umemejua kusambazwa Kisiwani Rukuba, RUWASA
itaendelea na mradi wake wa kusambaza maji ya bomba kisiwani humo.
Kuhusu elimu Kisiwa cha Rukuba kina Shule ya Msingi yenye
Maktaba na nyumba za makazi ya walimu wote. Upungufu wa vyumba vya madarasa
haupo tena.
Kama hiyo haitoshi jimbo hilo ambalo kipaumbele chake namba
moja ni elimu linajenga Sekondari mpya Kisiwani humo, na imepangwa ifunguiliwe
mwaka huu, 2025.
Kwa upande wa afya taarifa hiyo ya mbunge wa Jimbo la Musoma
Vijijini inasema kwamba kituo cha afya kimeanza kutoa huduma za matibabu na kimefungiwa
umemejua (solar energy).
0 Maoni