Papa Francis akutwa na dalili za awali za tatizo la figo

 

Papa Francis hali yake bado si nzuri, lakini hajaonyesha dalili za ziada katika mfumo wake wa kupumua, taarifa ya Vatican iliyotolewa Jumapili imesema.

Papa bado anaendelea kupatiwa tiba kwa kutumia mfumo wa oksijeni na kuwekewa damu. Pia vipimo vya damu vimeonyesha anadalili za awali za tatizo la figo, ila kwa sasa imedhibitiwa.

Taarifa ya Vatican imesema kuwa kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki Duniani anajitambua na anaendelea vyema.

Chapisha Maoni

0 Maoni