Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Mohamed
Mchengerwa, amefiwa na baba yake Alhaj Omary Mchengerwa leo alfajiri akiwa
kwenye Ibada ya Umrah huko Makka.
Kwa mujibu wa taarifa ya Familia ya Mchengerwa, Mzee Omary
atazikwa leo huko huko Makka.
Familia ya Mhe. Mchengerwa imetoa Ratiba ya Ibada ya visomo
vitakavyoongozwa na Mufti wa Tanzania Dkt. Zuberi Bin Ali wa Mbwana nyumbani
kwa Waziri Mchengerwa, Masaki Dar es Salaam.
LEO: TAREHE 24 FEBRUARI 2025
Dua ya Kisomo itafanyika nyumbani kwa Mhe. Mohamed
Mchengerwa Masaki saa 10 Alasiri
KESHO TAREHE: 25 FEBRUARI 2025
Dua ya kisomo itafanyika Jimboni Rufiji
KESHO KUTWA TAREHE: 26 FEBRUARI 2025
Dua itafanyika nyumbani kwake Marehemu Alhaj Omary Mchengerwa Yombo
0 Maoni