Kiongozi Mkuu wa 49 wa Madhehebu ya Shia Ismailia na
mwanzilishi wa Mtandao wa Maendeleo wa Aga Khan (AKDN), Mtukufu Aga Khan,
amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 88.
Mtukufu Aga Khan anayefahamika kama Karim Al-Hussaini Aga
Khan IV, amefariki dunia jana Februari 4, 2025, jijiji Lisbon, Ureno akiwa
amezungukwa na familia yake.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi kwa umma, baada ya kifo cha
kiongozi huyo, Imamu wa 50 wa madhehebu ya Shia Ismailia atatangazwa kurithi nafasi
ya Aga Khan IV.
Wakati wa uhai wake, Mtukufu Aga Khan alifahamika kutokana
na mchango wake kwenye shughuli zinazochangia kuimarisha ustawi wa maisha ya
binadamu katika maeneo mbalimbali duniani.
Mtukufu Aga Khan ameacha alama isiyofutika maeneo mbalimbali
duniani hususan katika nchini Kenya na Tanzania ambako alianzisha taasisi
mbalimbali zilizoleta mchango mkubwa katika maisha ya raia wa nchi hiyo.
Uwepo wa Aga Khan nchini Tanzania unaonekana kupitia uanzishwaji wa kampuni mbalimbali ikiwemo ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Hospitali za Aga Khan na miradi mbalimbali katika sekta ya afya na elimu.
0 Maoni