Wezi Wamarekani nao noma waiba mayai laki moja

 

Wezi wameiba mayai 100,000 yenye thamani ya dola za Marekani 40,000 sawa na shilingi milioni 101.6 za Tanzania katika jimbo la Pennsylvania nchini Marekani.

Polisi wa Marekani wizi huo wa mayai yaliyokuwa yakipelekwa sokoni umefanywa kwa wezi kuyapakua mayai kwenye lori huko Greencastle, Februari mosi.

Wizi huo umetokea wakati ambao bei ya mayai imepanda huku kukiwa na homa ya mafua ya ndege, na kuyafanya mayai kuwa na gharama kubwa.

Bei za mayai zimepanda zaidi ya 65% katika mwaka uliopita, kwa mujibu wa taarifa ya serikali ya Marekani. Idara ya kilimo ilitabiri gharama ya mayai itaongezeka kwa 20% mwaka 2025.

Chapisha Maoni

0 Maoni