Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) imesema kuanzia
mwezi Machi mwaka huu wa 2025 itasitisha rasmi matumizi ya tiketi za karatasi
katika usafiri wa Mabasi Yaendayo Haraka na badala yake watumiaji wote wa mabasi
hayo watatakiwa kutumia kadi janja ambazo zinaendelea kuuzwa katika vituo vikuu
vya mradi huo.
Akiongea Jijini Dar es Salaam wakati wa kuhitimisha mradi wa
maendelezo yatokanayo na uboreshaji wa usafiri wa umma (TOD), Mtendaji Mkuu wa
DART, Dkt. Athumani Kihamia amesema ifikapo Machi mosi matumizi ya tiketi za
karatasi katika kulipia nauli za mwendokasi yatasitishwa.
Dkt. Kihamia amesema matumizi ya kadi yanaondoa usumbufu wa kukosekana kwa chenchi lakini pia ni njia muafaka ya kudhibiti uvujaji na upotevu wa mapato ya Serikali.

0 Maoni