Wizara ya
Maliasili na Utalii imeandaa operesheni maalum ya doria inayoendelea
Wilayani Itilima kudhibiti fisi
katika maeneo hayo inayoshirikisha Askari wa Uhifadhi na wananchi wa maeneo hayo kwa siku kadhaa sasa.
Kwa mujibu wa
Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori wa Maliasili na Utalii, Dkt. Alexander
Lobora doria ya kudhibiti fisi inaendelea katika eneo la milima ya Kagera,
Kijiji cha Itilima, Kata ya Nyamalapa, Wilaya ya Itilima lengo ni kudhibiti
fisi hao wanaodaiwa kuwasumbua wananchi katika maeneo yote ya wilaya hiyo.
"Lengo
la doria hii ni kufanya ukaguzi kwenye eneo la milima hiyo ambapo inadaiwa na
wananchi wa eneo hilo kuwa ni maficho ya fisi," amesisitiza Dkt. Labora.
Aidha,
amefafanua kuwa doria maalum kama hizo ni endelevu kwa maeneo yote nchini
ambapo yataonekana kuwa na wanyama hatarishi kwa jamiii ili kuwalinda wananchi
wasiweze kusumbuliwa.
Amesema
katika doria hiyo, Mwenyekiti wa kijiji cha Lali Kata ya Lagangabilili wilaya
ya Itilima Kija Genge amewaongoza wananchi wake kushirikiana kwenye doria na
kikosi maalum cha Askari wa Uhifadhi wa Maliasili na Utalii katika eneo la
milima ya Lali.
Katibu Mkuu
wa Maliasili na Utalii, Dkt.Hassan Abbasi amefafanua kwamba Wizara itaendelea
kutekeleza mikakati ya kukabiliana na wanyama wakali na wahalibifu katika
maeneo yote nchini na ametoa wito kwa wananchi kutoa taarifa pindi
wanaposumbuliwa ili waweze kupata msaada
wa haraka wakati wowote.
"Wizara
imejipanga kikamilifu kukabiliana na wanyama wakali na wahalibifu wakati
wowote, hii kwetu kama Serikali ni
ajenda ya kudumu," amefafanua, Dkt. Abbasi.
Na. John
Mapepele- Itilima




0 Maoni