Halmashauri
ya Wilaya ya Busokelo imefanikiwa kutoa Mikopo ya Asilimia 10 kama takwa la
kisheria na maelekezo ya Mh. Rais Samia Suluhu Hassan kwa vikundi vya wanawake,
vijana na watu wenye ulemavu.
Mkurugenzi wa
Halmashauri hiyo Dkt. Mwinyi Omary
Mwinyi amesema jumla ya Kiasi cha Shilingi Milioni 177 zimetolewa kwa vikundi
hivyo Februari 06/02/2025 ikiwa ni awamu
ya kwanza ya kutoa mikopo.
Aidha, Dkt.
Mwinyi ameeleza kuwa awamu ya pili imeanza kwa usaili wa vikundi mbalimbali
kuanzia tarehe 02-30/02/2025 ambapo jumla ya shilingi milioni 500 zinatarajiwa
kutolewa kwa vikundi vitakavyopitishwa.
0 Maoni