Rais wa
kwanza wa Namibia huru, Sam Nujoma, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 95
katika mji mkuu wa Windhoek, kiongozi wa sasa wa nchi hiyo Nangolo Mbumba ametangaza.
Nujoma alikua
rais mwaka 1990 na aliongoza nchi hadi 2005, baadatu ya nchi hiyo kupata uhuru.
Nujoma
aliongoza vita vya muda mrefu vya kudai uhuru kutoka kwa Afrika Kusini mwaka
1990 baada ya kusaidia kupatikana kwa vuguvugu la ukombozi la Namibia
lililojulikana kama South West Peoples' Organization (SWAPO) miaka ya 1960.
Nujoma
alikuwa amelazwa hospitalini kwa muda wa wiki tatu zilizopita kutokana na
ugonjwa ambao "hakuweza kupona", Rais Mbumba amesema katika taarifa
yake akitangaza kifo hicho kwa "huzuni na masikitiko makubwa".
0 Maoni