Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.
Samia Suluhu Hassan amesema kuwa ameshtushwa na kuhuzunishwa na taarifa za kifo
cha rais wa kwanza wa Namibia baaada ya uhuru na Baba wa Taifa hilo Sam Nujoma.
Katika salamu
zake za pole, Rais Samia amesema kuwa Nujoma alikuwa ni mpigania uhuru,
mwanamajumui wa Afrika na raifiki wa Tanzania ambapo aliishi wakati wa harakati
wa kudai uhuru wa Namibia.
“Nujoma
aliishi maisha ya si tu ya kujenga mustakabali wa taifa lake, bali alivivutia vizazi
vya waafrika katika kusimamia dhana za uhuru, usawa na haki,” amesema Rais
Samia kupitia akaunti yake ya Instagram.
Amemalizia
kwa kusema kwamba, kwa niaba ya Serikali na watu wa Jumhuri ya Muungano wa
Tanzania, anatoa salamu za pole kwa Rais wa Namibia Dk. Nangolo Mbumba,
wananchi wa Namibia na Mke wa marehemu Kovambo Nujoma, watoto wake, familia
yote, marafiki na komredi wa SWAPO.
0 Maoni