Wataalam sekta za Wanyamapori na Misitu Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania,Wizara ya Maliasili na Utalii na Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili
na Mifugo kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakutana Jijini Arusha,
kujadili utekelezaji wa mashirikiano baina ya pande mbili kwa ustawi wa
uhifadhi na kukuza utalii nchini.
Wakizungumza wakati wa kikao hicho viongozi wa pande zote
mbili, Bi. Kay Kagaruki, Mkurugenzi Msaidizi Matumizi Endelevu ya Wanyamapori,
kutoka Wizara ya Malisili na Utalii, Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Bw.
Said Juma Ali Mkurugenzi wa Misitu, Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na
Mifugo Serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar wamesema mashirikiano hayo yameleta
tija katika sekta ya uhifadhi wa wanyamapori, Misitu na Utalii.
Aidha, miongoni mwa mada zilizojadiliwa katika kikao kazi hicho ambacho kimefanyika makao Makuu ya
TAWIRI, ni pamoja na utekelezaji wa Mikataba ya Kikanda na Kimataifa, udhibiti
wa ujangili, utoroshwaji wa nyara, usimamizi wa rasilimali za misitu, nyuki na
wanyamapori, utafiti na biashara katika sekta za misitu, nyuki na wanyamapori
na uendelezaji Utalii.


0 Maoni