Taasisi ya Makumbusho ya Taifa la Tanzania (NMT) imesema
kuwa imejiandaa kutumia fursa ya ugeni wa Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi
za Afrika kunadi vivutio pamoja na historia ya Taifa la Tanzania kwa wageni
hao.
Kauli hiyo imetolea leo na MNT, kwenye mahojiano
yaliyofanyika kwenye kituo cha televisheni cha Star TV yaliyowashirikisha Mhifadhi
historia Bw. Shomari Rajabu na Afisa Utalii Bi. Antonia Mnkama.
Kupitia mkutano huo utakaofanyika tarehe 27 na 28 Januari
jijini Dar es Salaam, Makumbusho ya Taifa la Tanzania imejipanga kuwatembeza
wageni wa mkutano huo katika maeneo ya kihistoria yanayopatikana jijini Dar es
Salaam ikiwemo vituo vyake vya Kijiji cha Makumbusho na Nyumba ya utamaduni.
0 Maoni