Serikali
ya Tanzania imeihakikishia Serikali ya Uingereza kuendeleza ushirikiano kwenye
sekta ya madini hususani katika kujengea uwezo watu wake, kubadilishana uzoefu,
uongezaji thamani madini na kuwekeza kwenye kufanya tafiti mbalimbali ili
kukuza sekta ya madini na kupanua mnyororo wa thamani ili kuongeza ajira na
kuchangia katika ukuaji wa pato la taifa.
Hayo,
yameelezwa Jana na Waziri wa Madini, Mh. Anthony Mavunde katika ofisi ndogo za
Wizara ya Madini jijini Dar es Salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na
Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Mhe. Marianne Young.
"Kwanza
kabisa Mhe. Balozi Young amefika ofisini kujitambulisha kwakuwa ana muda mfupi
nchini tangu awasili lakini pia tumezungumzia ushirikiano mkubwa uliopo kati ya
Tanzania na Uingereza.”
Katika
mazungumzo hayo, Tanzania na Uingereza zimekubaliana katika kuwajengea uwezo
watu wake na kubadilishana uzoefu hususani katika Taasisi ya Jiolojia na
Utafiti wa Madini nchini (GST) na British Geological Survey (BGS)ya Uingereza
ili kuwajengwa uwezo Watanzania kwakuwa na ujuzi stahiki katika masuala ya
uendelezaji wa sekta ya madini.
Eneo
la pili tulilozungumzia kwa urefu ni katika madini mkakati ambapo Uingereza
wameonesha utayari katika kushirikiana na Tanzania katika eneo la mnyororo
mzima wa uongezaji thamani madini mkakati ambapo Tanzania imejipanga
kuhakikisha inavutiwa uwekezaji mkubwa wa ujenzi wa viwanda vya kuongeza
thamani madini hapa nchini.
Sasa
ni muda muafaka wa kuhakikisha madini ya kimkakati yanawanufaisha Watanzania na
taifa, na ndiyo maana tumeandaa Mkakati maalumu wa kutekeleza azma hiyo huku
ikizingatiwa kuwa madini hayo kwa sasa yana mahitaji makubwa duniani.
Tupo
katika hatua za mwisho kukamilisha mkakati huu maalum wa madini mkakati na
muhimu ambao pia ni sehemu ya Kampeni ya Dunia katika kupunguza hewa ya ukaa
kupitia matumizi ya nishati safi," amesema Waziri Mavunde.
Akizungumza
katika Mkutano huo Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Mh. Marriane Young
amesema Uingereza inapongeza jitihada kubwa za kukuza sekta ya madini
zinazofanywa na serikali ya Tanzania chini ya Uongozi wa Mh. Rais Dkt. Samia S.
Hassan na kuahidi kuimarisha ushirikiano mkubwa baina ya nchi hizi hasa katika
kubadilishana uzoefu na kujengeana uwezo kupitia Taasisi za madini nchini
Uingereza na Tanzania.
Balozi
Young ameunga mkono mpango wa uongezaji thamani madini nchini na kuahidi kwamba
Uingereza itashirikiana na Tanzania kwa ukaribu ili
malengo hayo yatimie.
0 Maoni