Takribani
watu 126 wamekufa na wengine 188 wamejeruhiwa, baada ya tetemeko la ardhi
kupiga vilima vya Himalaya siku ya Jumanne, kulingana na vyombo vya habari vya
serikali ya China.
Wafanyakazi
wa uokoaji wanafukua vifusi kutafuta manusura baada ya tetemeko hilo
lililoharibu zaidi ya majengo 1,000 katika eneo la Tibet, karibu na mlima wa
Everest.
Operesheni
kubwa ya uokoaji inaendelea, huku walionusurika wakiwa chini ya shinikizo la
ziada kutokana na hali ya joto kufikia nyuzijoto 16.
Matetemeko
ya ardhi ni ya kawaida katika eneo hilo, kutokana na jiografia yake, lakini
tetemeko hilo limeacha vifo vya watu wengi zaidi nchini China katika miaka ya
hivi karibuni.
Tetemeko
hilo la ukubwa wa alama 7.1, ambalo lilipiga kwa kina cha kilomita 10,
kulingana na data kutoka Geological Survey ya Marekani, pia lilisikika nchini
Nepal na na sehemu za India, ambazo ni jirani na Tibet.
0 Maoni