Maelfu ya watu kuhamishwa kuepuka moto wa nyika Los Angeles

 

Mamlaka ya Los Angeles imetangaza hali ya tahadhari kutokana na moto wa nyika ulioanza kuunguza ekari 10 kushika kasi na kuteketeza ekari 2,900 kwa saa kadhaa.

Mkuu wa Kikosi cha Zimamoto Kristin Crowley ameagiza kuhamishwa watu zaidi 30,000, huku moto mwingine ukitokea katika maeneo mawili kaskazini magharibi mwa mji huo.

“Sikuwahi kuona siku kama hii, wakazi wanaangalia miale ya moto hawajui pa kwenda”, amesema mwandishi wa BBC, aliyepo Los Angeles.

Picha za mjongeo zinaonyesha nyumba zikitiketea kwa moto katika eneo la Pacific Palasades na wakazi wakitelekeza magari yao kukimbia miale ya moto.

Chapisha Maoni

0 Maoni