Kijiji cha Muhoji kimeamua kujenga sekondari
yake ili kutatua tatizo la umbali mrefu wanaotembea watoto wa kijiji hicho kwenda
masomoni kwenye Sekondari ya Kata iliyopo Kijijini Masinono.
Taarifa iliyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Musoma
Vijijini Prof. Sospeter Muhongo imesema Muhoji Sekondari ipo tayari, mwezi huu
(Januari 2025) kuanza kupokea wanafunzi wa Kidato cha Kwanza kutoka kijijini
humo.
Kukamilika kwa ujenzi wa sekondari hiyo iliyojengwa kwa nguzu ya wanakijiji, kutasaidia kuondokana na adha ya wanafunzi kutembea umbali mrefu wa kilomita kumi kwenda sekondari ya kata, imesema taarifa hiyo.
Ujenzi wa sekondari hiyo ulianza kwa kupitia
Harambee za Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof. Sospeter Muhongo, ambae amechangia
fedha zake binafsi.
Prof. Muhongo amesema, Mfuko wa Jimbo umechangia
baadhi ya vifaa vya ujenzi, Wanakijiji wamechangia fedha za ujenzi na nguvukazi
zao. Serikali nayo imetia mkono kwa kuchangua shilingi milioni 75.
Sekondari hii mpya, kwa miaka ya karibuni,
itapokea wanafunzi kutoka vijiji jirani vya Kaburabura (Kata ya Bugoji),
Saragana (Kata ya Nyambono) na hata wanafunzi kutoka Wilaya ya Bunda, Kitongoji
jirani sana cha Kinyambwiga.
Hadi sasa Muhoji Sekondari imekamilika ujenzi
wa vyumba vya madarasa vitatu, ofisi moja, vyoo: matundu 8 wasichana, na 6
wavulana, chumba cha maktaba pamoja na chumba cha huduma ya kwanza (matibabu).
0 Maoni