Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko Januari 10, 2025 amesema kuwa ukuaji wa uchumi wa nchi yoyote unategemea upatikanaji wa nishati ya uhakika na yenye gharama nafuu.
"Kwa nchi yoyote inayotaka kukua kwa
kiasi kikubwa inategemea Nishati inayopatikana kwa hakika na yenye bei nafuu,
Bila nishati ya gharama nafuu, uchumi utabadilika na bidhaa zitazalishwa kwa
gharama kubwa zaidi," amesema Dkt. Biteko.
Dkt. Biteko amesisitiza kuwa serikali
imejipanga kuhakikisha umeme wa uhakika unapatikana kwa gharama nafuu ili
kuchochea Maendeleo ya kiuchumi na kuboresha maisha ya wananchi.
0 Maoni