Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Januari 10, 2025 amewasili Kampala nchini Uganda ambako kesho atamwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika Mkutano kuhusu Mpango wa Kilimo Afrika utakaofanyika kwenye ukumbi wa hoteli ya Speke Resort and Conference Centre Munyonyo. Pichani, Waziri Mkuu akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Meja Jenerali Paul Kisesa (kushoto) alipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe. wa pili kushoto ni Balozi wa Uganda nchini, Kanali Mstaafu , Fredy Mwesigye. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozwa na Waziri wa Nchi anayeshugulikia Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Uganda, Fredrick Bwino Kyakulaga (wa pili kushoto) alipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe nchini Uganda Januari 10, 2025 ambako atamwakilisha Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika Mkutano kuhusu Mpango wa Kilimo Afrika utakaofanyika kwenye ukumbi wa hoteli ya Speke Resort anda Conference Centre Munyonyo Januari 11, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Nchi anayeshughulikia Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Fredrick Bwino Kyakulaga alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe nchini Uganda ambako atamwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika Mkutano kuhusu Mpango wa Kilimo Afrika utakaofanyika kwenye ukumbi wa hoteli ya Speke Resort and Conference Centre Munyonyo Januari 11, 2025. Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Meja Jenerali Paul Kisesa na kulia ni Balozi wa Uganda nchini Tanzania, Kanali Mstaafu Fredy Mwesigye. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
0 Maoni