Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa
ameeleza kuwa Kikosi maalum cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa Kushirikiana
na Wananchi kinaendelea na Operesheni ya kuwatafuta na kuwaokoa Wavuvi katika
Ziwa Rukwa ambapo kufikia jana tarehe 25 Januari 2025 saa tisa mchana, miili ya
Wavuvi nane imepatika.
Bashungwa akiwa ameambata na Waziri Wa Mifugo na Uvuvi, Dkt.
Ashatu Kijaji, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Edwin Mhede
kutoa pole kwa Wananchi wa Nankanga, ameeleza kuwa kufuatia upepo mkali
uliotokea mnamo tarehe 23 Januari 2025 na kuwakuta Wavuvi 550 wakiwa katika
shughuli zao ambapo jitiada za awali zilifanikiwa kuwaokoa Wavuvi 540 wakiwa
salama.
“Kwa taarifa tulizozipata sasa, pamoja na jitihada nzuri za
mafanikio tuliyopata ya kuokoa ndugu zetu 540 ambao tumewaokoa kutoa ziwani
kutokana na takwimu tulizokuwa nazo jana, lakini bahati mbaya kwa taarifa
nilizo nazo sasa kutoka kwa wanaonendelea ukoaji ziwani tumewapoteza ndugu zetu
saba” ameeleza Bashungwa saa sita mchana.
Bashungwa ameeleza zoezi za ukoaji linaendelea likiongozwa
na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji CGF John Masunga ambae
anatumia helkopta kuwasiliana Vikosi maalum vya uokoaji ambao wanashirikiana na
Wananchi ambao wana jumla ya vyombo 19.
Bashungwa ametoa wito kwa Wananchi na Watanzania kufuatilia
na kuzingatia taarifa zinatolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa kwa sababu Rais,
Dkt. Samia ameiwezesha mamlaka ya Hali ya Hewa kuwa na vifaa vya kisasa
vinavyotoa taarifa za uhakika kwa wakati.
Aidha, Bashungwa ameeleza kuwa Rais Dkt. Samia anaendelea
kuimarisha Jeshi la zimamoto na Uokoaji ili kuteleleza majukumu yake kwa
ufanisi ambapo ameliwezesha Jeshi hilo linanunuq helikopta moja ya kuokoa na
kuzima moto, magari 150 ya kuzima moto, magari 40 ya kubebea wagonjwa na boti
23 za kuzima moto na uokoaji.
Kwq upande wake, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na
Uokoaji, CGF John Masunga ameeleza kuwa Oparesheni ya Ukoaji itaendelea vizuri
kwa kuhakikisha wavuvi wote waliokuwa ziwani wanapatikana wakiwa hai au kupata
miili yao.
GGF Masunga amesema Kikosi Maalum cha Askari cha Uokoaji
kutoka Dar es salaam kitafika hapo Nankanga kuongeza nguvu ya uokozi kwa
kushirikiana Kikosi na Wananchi wanaoendelea na shughuli hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Sumbwanga Nyakia Chirukile amesema Zoezi
la Wananchi kuitambua miili ya ndugu zao linafanyika katika Zahanata ya kijiji
Nankanga ili kuwezesha taratibu za mazishi kufanyika.
Awali, Diwani kata ya Nankanga, Anyisile Kayuni ametoa shukrani kwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa faraja na upendo mkubwa kwa Wananchi kwa kuwaagiza Mawaziri kuja na vikosi maalum kuweka kambi na kuhakikisha ukoaji unafanyika pamoja na shughuli nyingine.




0 Maoni