Watu 11 wamefariki dunia baada ya lori lililokuwa limebeba saruji kufeli breki na kugonga watu waliokuwa wakisaidia majeruhi wa ajali ya basi aina ya Tata katika Kijiji cha Changombe, Kata ya Segera, Wilayani Handeni, Mkoa wa Tanga.
Lori hilo lenye namba za usajili T 680 BQW, likiwa linatokea
Tanga, lilifeli breki usiku wa kuamkia leo na kuwagonga watu waliokuwa
pembezoni mwa barabara na kusababisha vifo vya watu 11 papo hapo na kujeruhi
wengine 13.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Batilda Burian, amethibitisha
kutokea kwa ajali hiyo akisema kuwa tukio hilo ni la kusikitisha kwa sababu
waliofariki walikuwa wakijaribu kuwasaidia majeruhi wa ajali ya awali.
Balozi Batilda ametoa pole kwa familia za marehemu na kuwatakia nafuu ya haraka majeruhi wote na ametoa wito kwa madereva na wamiliki wa vyombo vya moto kuhakikisha magari yao yanakuwa katika hali nzuri ya kiufundi ili kuepusha ajali za namna hii.
0 Maoni