Rais Samia aiahidi Zanzibar Heroes Goli la Mama

 

Rais Samia Suluhu Hassan ameipongeza Zanzibar Heroes kwa kufanikiwa kufika hatua ya fainali ya Kombe la Mapinduzi na kuahidi katika mchezo wa fainali kutakuwa na zawadi ya fedha za Goli la Mama.

Rais Samia ametoa pongezi hizo kupitia akaunti yake ya mtandao wa Instagram, kwa kuandika yafuatayo:-

Ninaipongeza Zanzibar Heroes kwa kufanikiwa kufika hatua ya fainali ya Mashindano ya Kombe la Mapinduzi. Mmejitoa, mmejituma na sote tunajivunia safari yenu hadi sasa.

Mchezo huu wa fainali ni nafasi ya kipekee kwenu kuandika historia, nasi tuko nyuma yenu kuwaunga mkono.

Ninawatakia kila la kheri, na ninawaahidi katika mchezo huu wa fainali Goli la Mama litakuwepo.

Chapisha Maoni

0 Maoni