Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imeridhishwa na utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zake kwa namna inavyowagusa wananchi, huku ikimpongeza Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa juhudi zake za kukuza ustawi na maendeleo ya Watanzania.
Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo,
Fatuma Toufiq, jana Januari 21, 2025, jijini Dodoma wakati ikipokea taarifa ya
utekelezaji wa mpango na bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira
na Wenye Ulemavu kwa kipindi cha Julai hadi Desemba 2024.
Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu –
Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete, amesema ofisi hiyo
katika mwaka wa fedha 2024/2025 imepanga kuendelea kutekeleza shughuli
mbalimbali, zikiwemo usimamizi wa kazi na huduma za ukaguzi, maendeleo ya
vijana, kuratibu shughuli za ajira, utoaji wa huduma kwa watu wenye ulemavu,
hifadhi ya jamii, na ukuzaji wa tija. Ameahidi kuwa ofisi hiyo itatekeleza
majukumu hayo kikamilifu ili kufanikisha malengo yaliyowekwa.



0 Maoni