Tundu Lissu ametangazwa kuwa mshindi wa nafasi ya
Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), katika
uchaguzi uliofanyika jana usiku.
Akitangaza matokeo hayo leo na Mwenyekiti wa Uchaguzi Prof.
Raymond Mushi amesema, wapigakura waliojisajili walikuwa 1,014 kura
zilizopigiwa ni 999, halali zikiwa 996 na tatu zimeharibika.
Prof. Mushi ameeleza kuwa Odero Odero kapata kura moja
sawa na asilimia 0.1, Freeman Mbowe amepata kura 482 sawa na asilimia 48.3 huku
Lissu akipata kura 513 sawa na asilimia 51.5.
Kwa upande wa Nafasi ya Makamu Wenyekiti wa Chadema
Zanzibar ameshinda Said Mzee Said ambaye amepata kura 625 sawa na asilimia 89
ya kura 706 huku kura halali zikiwa 700 na sita zimeharibika.

0 Maoni