Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa leo
tarehe 22 Januari 2025 amewasili Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Dodoma na
kupokelewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP. Camillus Wambura pamoja na
Makamishna wa Jeshi hilo.
Katika ziara hiyo ya kwanza ya Kikazi katika Jeshi la
Polisi tangu alipoteuliwa na Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Waziri Bashungwa amepokelewa kwa salamu ya
gwaride la heshima (Mounted Guard).
Pamoja na Mambo mengine, Waziri Bashungwa atafanya kikao
na kuzungumza na Maafisa, Wakaguzi, Askari wa vyeo mbalimbali na watumishi
wengine wa Jeshi la Polisi.



0 Maoni