Waziri wa
Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) amekutana na kufanya
mazungumzo na Ujumbe kutoka Ujerumani ukiongozwa na Mkurugenzi anayeshughulikia
Masuala ya Kusini mwa Jangwa la Sahara na Sahel kutoka Wizara ya Mambo ya Nje
ya Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani, Mhe. Christoph Retzlaff.
Lengo ikiwa
ni kujadiliana masuala mbalimbali ya ushirikiano baina ya Tanzania na Ujerumani
hususan uhifadhi wa mazingira asili na mienendo ya miradi mbalimbali
inayohifadhiliwa na Serikali ya Ujerumani kupitia Wizara ya Maendeleo BMZ.
Kikao hicho
kimefanyika leo Desemba 05,2024 katika ukumbi wa Chuo cha Taifa cha Utalii
jijni Dar es Salaam.
Pamoja na
mambo mengine kikao hicho kilijadili kuhusu kushirikiana katika maeneo ya
Urithi wa Utamaduni wa Kikoloni
(colonial heritage), Makumbusho ya Taifa na ushirikiano baina ya nchi hizo
katika bioanuai.
Akizungumza
katika kikao hicho, Mhe. Chana aliipongeza Ujerumani kwa namna ambavyo imekuwa
ikitoa ufadhili nkatika miradi mbalimbali ya
katika Sekta ya Maliasili na Utalii nchini Tanzania ambayo imepelekea
kukua kwa Sekta hiyo ambapo kwa sasa inachangia asilimia 17 katika Pato la
taifa na asilimia 25 kwa fedha za kigeni.
“Uwepo wa
watalii nchini umeongeza ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja
nchini ikiwemo kuwawezesha wajasiriamali wadogo kuongeza vipato vyao madereva
tax, wauzaji wa vyakula na watoaji wa huduma za malazi hunufaika,” Mhe. Chana
amesema.
Kwa upande
wake, Mkurugenzi anayeshughulikia Masuala ya Kusini mwa Jangwa la Saharana
Sahel kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani,
Christoph Retzlaff alisema kuwa Tanzania
ni mshirika muhimu wa Ujerumani na
Ujerumani ina nia ya kujenga uhusiano katika maeneo mengi zaidi hasa katika
bioanuai(biodiversity).
Kikao hicho
kimehudhuriwa na Balozi was Shirikisho la Ujerumani Tanzania, Mhe. Thomas
Terstegen Balozi wa Tanzania nchini
Ujerumani, Mhe. Hassan Mwamweta, Mkurugenzi
Msaidizi Idara ya Ulaya na Amerika kutoka Wizara ya Mambo ya Nje, Gerald
Mbwafu, Afisa Mambo ya Nje II, kutoka Wizara ya Mambo ya Nje. , Lisa Kilua, Mkuu wa
Ushirikiano, Bi. Julia Kronberg na Naibu Mkuu wa Ujumbe Bw.Manuel Müller,Mkurugenzi wa Makumbusho
ya Taifa Tanzania, Dkt. Noel Luoga na wawakilishi kutoka Bodi ya Utalii
Tanzania.
Na.
Happiness Shayo - Dar es Salaam
0 Maoni