Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linachunguza kifo cha mwanafunzi
wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), ambaye amekufa maji kwenye maporomoko ya maji ya
Sanje yaliyo katika Hifadhi ya Taifa ya Udzungwa Wilaya ya Kilombero Mkoa wa
Morogoro.
Tukio hilo limetokea jana Desemba 22, 2024 majira ya mchana
ambapo mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa UDOM Hezekiel Petro (21) anayesoma
masomo ya sanaa na historia alikufa maji baada ya kukanyaga jiwe lenye utelezi
na kutumbukia kwenye kina kirefu cha maji.
Mwanafunzi huyo alifika katika maeneo hayo akiwa kwenye ziara
ya mafunzo kwa vitendo na wanafunzi wenzake zaidi ya 300 wakiwa wamefuatana na
wakufunzi wao ambapo mwili wa mwanafunzi huyo ulitolewa kwenye maji na
wataalamu wa kuogelea.
Kufuatia tukio hilo Jeshi la Polisi Morogoro kupitia kwa RPC
Mkoa Morogoro SACP. Alex Mkama limetoa wito kwa wananchi wote kuchukua
tahadhari na kufuata maelekezo ya wataalamu wanapotembelea maeneo yenye upekee.
0 Maoni