Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara za VIjijini na Mijini (TARURA), Mhandisi Victor Seff amewashukuru Watanzania wote waliojitokeza na kumpigia kura wakati akiwania tuzo za Mtendaji/Mkurugenzi Mkuu Bora wa mwaka 2024 kati ya Wakurugenzi 100 walioteuliwa kuwania tuzo hizo (Top 100 Executive List Awards) na yeye kuibuka kinara.
Mhandisi
Seff ameyasema hayo leo tarehe 3/12/2024 jijini Dodoma wakati akiongea na
watumishi waTARURA Makuu mara baada ya kuwasili ofisi za Taasisi hiyo zilizopo
Mji wa Serikali Mtumba.
Mhandisi
Seff amewashukuru watumishi wote kwa ushirikiano wao katika utendaji kazi wa
Taasisi hiyo na hivyo kumfikisha hapo alipo "Hili sio jambo dogo, ni jambo
la kumshukuru Mungu sana. Naomba tuendelee kumshukuru Mungu ili Taasisi yetu
iendelee kufanya vizuri."
Aidha,
amewataka watumishi hao kuendelea kufanya kazi kwa ushirikiano ili kutimiza
malengo ya Serikali pamoja na kuendeleza yale ambayo yeye ameyafikia "Sasa
hivi tumepata sifa hii kubwa ila kazi kubwa tuliyonayo ni kuilinda sifa hii. Na
mimi naona timu iliyopo hapa inaweza kuilinda sifa hii iwe nipo au hata
nisipokuwepo,” amesema.
Hata hivyo,
amesema kwamba Serikali inaendelea kuthamini kazi kubwa inayofanywa na TARURA
hivyo amewasihi watumishi wote kuendelea kuchapa kazi ili kuhakikisha Taasisi inabaki
na sifa iliyopo.
Naye,
Mkurugenzi wa Barabara, Mhandisi Venant Komba amempongeza Mtendaji Mkuu huyo na
kusema kuwa Uongozi wake umekuwa ni msaada mkubwa kwa viongozi wengine wa chini
yake ambapo ameacha milango wazi wa kila mtumishi kumsikiliza muda wote na
kuahidi wataendelea kumpa ushirikiano katika majukumu yake.
Pia, Mhasibu
Mkuu, CPA. Jacob Nyaulingo amempongeza Mtendaji Mkuu kwa kuitwaa tuzo hiyo na
kumuelezea Mtendaji Mkuu kama mtu anayependa mabadiliko ambayo yamepelekea
kutengeneza mfumo wa malipo, mapato pamoja na uanzishaji wa hatifungani ya
miundombinu ya barabara (Samia Infrastructure Bond) ambayo inaenda kuwasaidia wakandarasi
wanaofanya kazi za ujenzi na matengenezo ya barabara za Wilaya zilizo chini ya
TARURA.
Akitoa
salamu kwa niaba ya Watumishi wa TARURA Mtunza Kumbukumbu Msaidizi, Bi. Sekela
Fumbo amempongeza Mtendaji Mkuu kwa kuchaguliwa kuwa 'CEO' Bora wa Mwaka 2024
na kuahidi kwamba watumishi wataendelea kufanya kazi kwa bidii, uadilifu na
uaminifu ili Taasisi izidi kufanya kazi vizuri zaidi ya hapo ilipo.
Wakati huo
huo, Dereva Mkuu, Bw. Assery Masawe amesema kwamba wanajivunia kumpata Kiongozi
ambaye anafanya kazi kwa kiwango kikubwa licha ya TARURA kuwa na muda mfupi
tangu kuanzishwa kwake, hivyo wanampongeza na kumtia moyo aendelee kuwaongoza
katika kuiendeza Taasisi yao vyema.
0 Maoni