Mkuu wa
Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania Jenerali Jacob John Mkunda kwa niaba
ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt Samia
Suluhu Hassan amewavisha nishani mbalimbali Majenerali, Maafisa na Askari wa
JWTZ jijini Arusha tarehe 02 Desemba 2024.
Nishani hizo
ni pamoja na Nishani ya Kumbukumbu ya Muungano Daraja la Nne, Nishani ya Utumishi
Uliotukuka, Nishani ya Utumishi Mrefu, Nishani ya Utumishi Mrefu na Tabia
Njema, na Nishani ya Miaka 60 ya JWTZ.
Aidha, Jenerali
Mkunda amewavisha nishani ya Jumuiya ya SADC Maafisa na Askari walioshiriki
Ulinzi wa Amani nchini Msumbiji chini ya mwavuli wa Jumuiya hiyo.
Akizungumza
na Wanajeshi Kanda ya Arusha, Jenerali Mkunda amemshukuru Mheshimiwa Rais Samia
kwa kuwatunuku Nishani hizo.
Aidha,
amewataka Wanajeshi kote Nchini Kuviishi Viapo Vyao walivyoapa, kufanya kazi
kwa Nguvu zote kwa Uhodari, Uaminifu, Utii na Nidhamu ili kuweza kuilinda Nchi,
kulinda Katiba na Kumtii Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na
Amiri Jeshi Mkuu.

0 Maoni