Wananchi wa
Kata ya Babati wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia
Suluhu Hassan kwa ujenzi wa madaraja saba (7) pamoja na kufungua barabara
katika kata hiyo ambapo kwa kipindi kirefu wamekuwa wakipata adha ya usafiri
hususan kipindi cha mvua.
Akitoa
pongeze hizo Diwani wa kata ya Babati Mhe. Haruni Msalu amesema kwamba
wanamshukuru Rais kwa kuwatendea haki Kata ya Babati kwani Kata hiyo ilikuwa na
makorongo mengi sana na kusababisha wananchi kuteseka hasa kipindi cha mvua na
hivyo kusababisha kusimamisha kwa muda shughuli zao za kila siku.
Amesema
katika kipindi cha Awamu ya sita Serikali kupitia TARURA imeweza kujenga
madaraja yapatayo saba katika Kata ya babati katika eneo la Amboni C, Kambi ya
Fisi, Hostel ya chuo cha uhasibu na Old Majengo-Angoni. “Old Majengo kuja
Angoni kulikuwa na kortongo kubwa ambalo lilikuwa likipitisha maji kwenda
ziwani, wananchi wakiwemo wanafunzi walikuwa wakipata tabu sana na hivyo
kuathiri utendaji kazi kwa wanafunzi na wafanyakazi kwani iliwapasa kusitisha
kwa muda kupita katika makorongo hayo.”
Mhe. Msalu
aliongeza kusema kuwa katika mpango wa TARURA wilaya ya Babati walitenga fedha
kwaajili ya kujenga madaraja pamoja na kufungua barabara “kwakweli niwapongeze
wafanyakazi wa TARURA kwa kutufungulia barabara kwani wananchi wa Babati njiji,
majengo, Kware na mtaa wa Angoni wananufaika na ujenzi huu,” alisema.
“Kwa bajeti
hii ya 2024/2025 tumeendelea kutatua changamoto ambapo daraja la
mnara-Kijiweni sasa hivi ujenzi
unakamilika na watu wameanza kupita lakini kazi ya kumwaga changarawe itaanza, niendelee kuwapongeza
TARURA kwani katika pindi cha miaka minne kwa kujenga madaraja saba ni kazi
kubwa sana na bado wanaendelea kutusikiliza na wananchi tupo na imani na
Serikali,” alisisitiza.
Hata hivyo
diwani huyo amesema wao kama viongozi kwenye kata wanaendelea kusimamia miradi
kwa kushirkiana na wataalam ili kuhakikisha wananchi wanaendelea kupata huduma
zinazostahili.
Naye, Bw.
Omary Nyange, Mkazi wa Mrara amesema
wanatoa shukrani nyingi sana kwa Serikali kwa kukamilisha ujenzi wa
madaraja kwa kumalizika Wilaya ya Babati
inapokea mazao mengi kutoka vijijini na biashara za mazao zinafanyika kwa wingi
hivyo kukamilika kwa madaraja hivi sasa hakuna changamoto yeyote na malighafi
zinaweza kufika mjini bila shida yeyote.
Ameongeza
kwamba kwa kukamilika kwa madaraja hayo hivi sasa wanafunzi wanaweza kupata
vipindi vyote vya masoko kwani hakutakuwa na kizuizi chochote katika makorongo
hayo katika kata.
Wakati huo
huo Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni Mkazi wa Mrara Bw. Hamis Rajabu amesema Ilani yao
imetekelezeka vizuri.
"Kwani
ujenzi wa madaraja hayo ambayo yalikuwa ni kiunganishi kati ya babati mjini na
vijijini, kero zote zimekwishwa hususan wale waendesha vyombo vya moto watakuwa
wamepata mkombozi."
"Poa
itatusaidia kutunyanyua kiuchumi kwani hakutakuwa na kitu kitakachowazuia
tusiendelee na kusafirisha mazao husuan kipindi cha mvua," amesema.
Pia Kaimu
Meneja wa TARURA wilaya ya Babati, Mhandisi Naftari Lyatuu amesema kukamilika
kwa mradi wa ujenzi wa madaraja makubwa mawili na madaraja matano madogo pamoja
na barabara ya babati-Mtuka (Km. 6) na barabara ya Nakwa (Km. 6) ambazo
zinaunganisha kata tatu ikiwemo vyuo vya veta, Uhasibu pamoja na hifadhi ya
taifa ya Tarangire kupitia geti la Mamile imeweza kufungua huduma nyingi za
kijamii pamoja na utalii kwani wakazi wengi wanaishi upande huo wa madaraja
yalipojengwa na hivyo kuweza kuwaunganisha na makao makuu
ya mji wa Babati.
0 Maoni