Bodi ya
Wakurugenzi ya Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA) imefanya ziara ya kikazi kijiji cha Msomera Handeni mkoani Tanga
kukagua utekelezaji wa ujenzi wa miundombinu mbalimbali kwa ajili ya wananchi
wa Ngorongoro wanaoendelea kuhamia eneo hilo.
Akiongoza
bodi hiyo Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi NCAA Jenerali Venance Mabeyo
(mstaafu) amezipongeza Sekta zote zinazohusika kutekeleza mradi huo kijiji cha
Msomera kwa kukamilisha Nyumba 2500, ujenzi wa miundombinu ya Maji,
mawasiliano, barabara, minada, majosho, kituo cha kuuzia maziwa, shule,
zahanati, shule, kutenga maeneo ya malisho na miundombinu mingine kijijini
hapo.
"Tumetembelea
eneo la Block F ambapo nyumba 1,000 zimekamilishwa katika awamu ya kwanza
iliyohusisha ujenzi wa Nyumba 5,000, kitalu hiki pekee kuna matenki matatu ya
maji yenye ujazo la lita laki 3 kwa kila moja, tenki lingine la ujazo wa lita
laki 650,000 linajengwa, hii inathibitisha kuwa wananchi wanaopisha shughuli za
uhifadhi Ngorongoro wakija hapa watafurahia maisha yao" ameongeza Jenerali
Mabeyo.
Akiambatana
na Bodi ya Wakurugenzi NCAA, Mkuu wa Wilaya ya Handeni Wakili Albert Msando
amewahakikishia wananchi wa Ngorongoro wanaohamia eneo hilo kuwa hali ya
usalama ni shwari, nyumba zimekamilika, huduma za kijamii zipo katika eneo lote
la Msomera na huduma zingine zinaendelea kujengwa ili kukidhi mahitaji ya
wananchi wanaohamia.
Kaimu
Kamanda wa Operesheni wa Ujenzi wa Nyumba 5000 za Msomera, Kitwai na Saunyi
Luteni Kanali Edward Mwanga ameieleza bodi hiyo kuwa SUMA JKT wamekamilisha
ujenzi wa Nyumba zote 2500 kwa asilimia 100 zikiwa katika kiwango cha kisasa na
ubora wa hali ya juu na wako tayari kwa kazi ya ujenzi wa Nyumba zingine 2,500
ambapo Nyumba 1000 zitajengwa kijiji cha Saunyi Wilaya ya Kilindi na Nyumba
1500 zitajengwa kijiji cha kitwai B Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara.
Mwakilishi
wa Kamishna wa Uhifadhi NCAA, SACC Gloria Bideberi amesema kuwa uongozi wa NCAA
utahakikisha kuwa kazi ya uelimishaji na uhamasishaji kwa wananchi inaendelea
kwa kasi zaidi ili wananchi waliopo Ngorongoro waendelee kuhamia Msomera.
Ameongeza kuwa kaya takribani 30 kutoka Ngorongoro zitahamishiwa katika kijiji
hicho mwisho wa mwezi Novemba,2024 baada ya kukamilisha uthamini na kulipwa
stahiki zao kwa mujibu wa sheria.
Na. Kassim Nyaki-
Msomera Tanga
0 Maoni