Jukwaa la
Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Mkoani Dodoma kwa kauli moja limempongeza Mh. Rais
Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweza mazingira mazuri ya ukuaji wa kiuchumi wa
wanawake pamoja na kuongeza fursa za kiuchumi mkoani Dodoma ambapo wananwake ni
kundi kubwa wanufaika.
Pongezi hizo
zimetolewa jana na Mwenyekiti wa Jukwaa Bi. Maryrhobi Mabhaya wakati wa
Kongamano la wakina Mama wa Dodoma kumpongeza Mh. Rais Samia kwa namna ambavyo
serikali ya awamu ya sita ilivyochochea maendeleo katika Mkoa wa Dodoma na
hivyo kutengeneza fursa kubwa ya kiuchumi.
“Dodoma ya
leo sio kama ya zamani, maendeleo ya Dodoma ya sasa huwezi kuyasema bila kumtaja
Rais Samia.”
“Hivi sasa
kuna fursa lukuki za kiuchumi ambazo wakinamama tukizitumia vizuri zitasaidia
kubadilisha uchumi wa wakina mama wa Dodoma. Sisi kama Jukwaa malengo yetu ni
kujenga eneo la maduka makubwa (Shopping Mall) pamoja na kuwa na eneo maalum la
biashara ta wakina mama,” alisema Maryrhobi.
Akimkaribisha
Mgeni Rasmi,Mlezi wa Jukwaa Mama Tunu Pinda amesema ni wakati sasa wanawake wa
Dodoma kutumia fursa hizi kubwa kiuchumi ambazo Mh. Rais Samia amekuwa kinara
wake kuzitengeneza hapa Dodoma ili kujiimarisha na kukua zaidi kiuchumi.
Akiwasilisha
hotuba yake,Mgeni Rasmi wa Kongamano hilo Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini na
Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde amesema tangu maamuzi ya kuhamishia
shughuli za serikali Dodoma,fursa nyingi za kiuchumi zimeongezeka na hivyo
serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi ili kuliona kundi kubwa la
wanawake likinufaika kupitia sheria na sera wezeshi.
Mavunde
alieleza kwamba, Mh. Rais Samia amerudisha mikopo ya wakina mama ya 10% na pia
Sheria ya Manunuzi ya Umma imefanyiwa marekebisho ili Taasisi nunuzi zitenge
30% ya manunuzi yake kwa ajili ya makundi maalum likiwemo kundi la wakina mama.
“Nitaendelea
kuunga mkono jitihada za kuwawezesha wanawake kiuchumi kwa vitendo,na mwaka huu
nitakabidhi kwa kikundi cha wakina Mama Ipagala mitambo ya kusafisha mafuta ya
Alizeti ambapo ni sehemu ya ahadi yangu ya uanzishwaji wa kiwanda cha kuongeza
thamani mazao kila mwaka,” alisema Mavunde.
Wanawake wa
Dodoma walitumia jukwaa hilo pia kumpa tuzo ya Mh. Anthony Mavunde kwa kutambua
mchango wake mkubwa kuwaendeleza wakina mama mkoani Dodoma.
0 Maoni