Watu kadhaa
wanahofiwa kuwa wamefukiwa na kifusi baada ya jengo moja la ghorofa lililopo
Kariakoo Mtaa wa Kongo na Mchikichi jijini Dar es Salaam kuporomoka.
Mashuhuda
wameeleza kuwa jengo hilo la biashara lileporomoka leo Jumamosi, ambapo
inahofiwa kuwa kuna watu walikuwamo katika eneo la chini wakati likiporomoka.
Wameeleza
kuwa kunawafanyabiashara na watu kadhaa walikokuwa wanafanya manunuzi katika
maduka ya jengo lililoporomoka.
Polisi kwa
kushirikiana na wananchi wanaendelea na jitihada za uokoaji, ili kunusuru maisha
ya watu waliofukiwa na kifusi.
0 Maoni